
Watu watano akiwemo Mganga wa kienyeji, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mara wakituhumiwa kumuua Mwalimu Monica Patrick (31), mkazi wa Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, ambaye aliuawa akiwa kwa mganga baada ya kunyweshwa dawa inayosadikika kuwa ni sumu na mganga huyo, ili imsaidie kupata fedha nyingi katika shughuli za uchimbaji wa madini, kisha mwili wake kutupwa kichakani katika Mtaa wa Kinyang'wena uliopo Manispaa ya Musoma.
