
Familia 40 za kijiji cha Komesha kata ya mfereji wilayani Monduli mkoani Arusha hazina makazi baada ya nyumba zao kuteketezwa kwa moto baada ya ya kuibuka kwa mgogoro wa kugombea mpaka unaounganisha wilaya za Arumeru na Monduli.
Baadhi ya wannchi wamesema hatua ya kuchoma nyumba hizo ilikuja baada ya kutokea kutoelewana miongoni mwa wananchi wa upande wa vijiji vya wilaya ya Arumeru na Monduli juu ya matumizi ya ardhi
Baadhi ya viongozi wa wilaya ya Monduli wamefika kwenye eneo hilo na licha ya kulazimika kufanyazi ya ziada ya kuwatuliza wananchi wa vijiji vya upande wa wilaya yao waliokuwa wanataka kwenda kulipiza kisasi wameiomba serikali kuu kumaliza mgogoro huo kwani jmbo linalowezekana.
Kufuatia hali hiyo Jeshi la polisi wialya ya Monduli limelazimika kuimarisha ulinzi huku mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Monduli akiwatahadharisha wananchi kuepuka kuchukua sheria mkononi.
Akizungumza kwa njia ya simu mkuu wa wilaya ya Monduli Bw Iddy Kimanta amesema kwa sasa hali ni shwari na kwamba jitihada za kutatua mgogoro huo zinaendelea zikihusisha wadau wa ngazi mbalimbali zikiwemo za mkoa na taifa.