Back to top

MGOMBEA KUTOKA UPINZANI ASHINDA URAIS SENEGAL

26 March 2024
Share

Mgombea wa Urais kutoka kambi ya upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye, ameshinda uchaguzi wa rais nchini humo ikiwa ni wiki moja baada ya kutoka gerezani, ambapo Mgombea wa Chama Tawala nchini humo, Amadou Ba amempongeza kwa ushindi huo.

Rais Mteule Bassirou Diomaye Faye mwenye miaka 44, anaweka historia ya kuwa Rais mwenye Umri mdogo zaidi Afrika.

Faye mpinzani wa viongozi walioko madarakani ameahidi kurejesha mamlaka ya nchi kupambana na ufisadi na kuleta uwiano wa kiuchumi.

Katika uchaguzi huo, maelfu ya raia wa senega walijitokeza katika maeneo mbalimbali nchini humo na waangaliazi kutoka mashirika mengi walikuwepo, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Ulaya, ambao ulituma waangaliazi 100 katika meneo mbalimbali nchini.

Uchaguzi huo umekuja baada ya hatua ya awali ya Rais anayeondoka madarakani Macky Sall, kutaka kuahirisha uchaguzi kuzua hofu ya kuwa anataka kujaribu kushikilia madaraka.