Back to top

Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan apokea hati za utambulisho za Mabalozi 5.

10 May 2021
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 10 Mei, 2021 amepokea hati za utambulisho za Mabalozi 5 walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha hati zao ni Mhe. Lebbius Taneni Tobias (Balozi wa Namibia hapa nchini), Mhe. Mary O’Nell (Balozi wa Ireland hapa nchini), Mhe. Dkt. Mehmet Güllüoglu (Balozi wa Uturuki hapa nchini), Mhe. Marco Lombardi (Balozi wa Italy hapa nchini) na Mhe. Ricardo Ambrosia Sampio Mtumbuida (Balozi wa Msumbiji hapa nchini).