Back to top

Miili ya watu 26 waliouawa kikatili na kuchomwa moto, yazikwa.

16 May 2018
Share

Serikali ya Burundi imeungana na wanakijiji cha Ruagarika mkoa wa Chibitoke kuzika miili ya watu 26 waliouawa kikatili kwa kupigwa risasi na maiti zao kuchomwa moto na kundi linalosadikiwa kuwa la waasi kutoka Congo  DRC.

Tukio hilo lililovuta hisia na kuleta simanzi kwa Warundi limehudhuriwa pia na mabalozi na wawakilishi wa Jumuiya mbalimbali za kimataifa huku Mwenyekiti wabaraza la kudhubiti machafuko nchini Burundi Bw.John Didi akilaani kitendo hicho na kutaka serikali ya Burundi na Jumuia ya Afrika Mashariki kuhakikisha wanatokomeza vikundi hivyo kwa maslahi mapana ya warundi na Afrika kwa ujumla.

Kwa mujibu wa taarifa ya Gavana wa jimbo hilo watu hao waliuawa na kikosi cha Askari Jeshi waliovuka mpaka kwa miguu wakiwa na silaha za kivita na kisha kushambulia kijiji hicho kwa kuuwa watu 26 na wengine kujeruhiwa.