Back to top

Milioni 780 zatolewa kujenga kliniki ya huduma za Methadone Tanga.

25 June 2020
Share

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wanaendelea kuboresha huduma za afya nchini ambapo shilingi milioni 780 zimetolewa kwa ajili ya kujenga kliniki ya huduma za methadone kwa waathirika wa dawa za kulevya mkoani Tanga.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa kituo cha muda cha kutoa tiba ya methadone kwa warahibu wa madawa ya kulevya kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo.