
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shighella ameagiza kukamatwa kwa mifugo inayochungiwa kwenye mashamba huku akitoa maagizo kwa pande zote mbili za wakulima na wafugaji kuacha kuingiliana kwenye maeneo yao.
Maagizo hayo ameyatoa wakati mkuu huyo wa mkoa alipo kuwa kwenye ziara ya kukagua mashamba ya Mkonge yaliyopo mkoani hapa na hapo ndipo alipokutana na makundi makubwa ya mifugo yakiwa kwenye mashamba hayo huku wamiliki wa mashamba hayo wakilalamikia hali hiyo.
Hata hivyo baadhi ya wamiliki hao wametoa pongezi kwa mkuu huyo kwa kuwatembelea kwani imepita miaka mingi bila kuona viongozi wa juu wakiwatembelea.
