Morrison kupelekwa Kamati ya Maadili.

Bernard Morrison ashinda kesi yake katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji (TFF) ambapo Mwenyekiti wa kamati hiyo Elias Mwanjala amesema wamebaini mapungufu katika mkataba wa Yanga na mchezaji huyo ikiwemo tarehe ya mkataba kuisha hivyo wamempa faida Morrison.

Hata hivyo mchezaji huyo atapelekwa katika kamati ya maadili kwa kosa la kusaini mkataba na Simba wakati bado sakata lake halijatolewa maamuzi.