Back to top

MSAADA WAKISHERIA UNARAHISISHA UPATIKANAJI HAKI.

10 April 2024
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa huduma ya utoaji wa msaada wa kisheria inayotolewa nchini inasaidia upatikanaji wa haki kwa wananchi wanaohitaki msaada katika kesi za jinai na kiraia.

Ili kufikia hilo Serikali ya Tanzania ilizindua Kampeni kubwa ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign-MSLAC).

 Kampeni hiyo inahusisha utoaji wa msaada wa kisheria na elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya kikatiba na kisheria, upatikanaji wa haki na masuala mtambuka kama vile ukatili wa kijinsia, ukatili dhidi ya wanawake na watoto, ardhi, mirathi, haki za binadamu kwa ujumla na utatuzi wa migogoro ikiwemo kuhamasisha utatuzi kwa kutumia njia mbadala.

"Baada ya kuona uhitaji mkubwa wa msaada wa kisheria serikali ilitoa wito kwa wadau wengine kuchukua jukumu katika kutoa msaada wa kisheria, na tunashukuru sana kwa sababu tuna watu wanaojitolea, watendaji wasio wa serikali, ambao pia hutoa msaada wa kisheria kwa watu,  Tunashukuru sana" -Rais Samia.