Back to top

Msinunue ardhi kupitia mifumo isiyo rasmi (Vishoka)

25 September 2022
Share

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewatahadharisha wananchi kuepuka kununua ardhi kupitia mifumo isiyo rasmi na kuwataka kujiepusha na matapeli wakiwemo vishoka na baadhi ya madalali ambao wamekuwa ni chanzo kikubwa cha migogoro ya ardhi nchini hali inayosabisha wananchi kupoteza haki ya msingi ya umiliki wa ardhi.
.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara hiyo Dkt.Allan Kijazi wakati akitoa taarifa kuhusu kampeni maalumu ya utatuzi wa migogoro ya ardhi.