Back to top

MTOTO ALIYESALIA MTUMBWI KUZAMA APATIKANA

02 March 2023
Share

Mwili wa mtoto Zainab Masoud (8) uliokuwa umesalia majini, hatimaye umepatikana baada ya ajali ya watoto wanne kuzama katika mto Luiche, Manispaa ya Kigoma Ujiji ,wakiwa wanaelekea shule wiki iliyopita.

Kaimu Kamanda wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kigoma ,Insipekta Jacob Chacha, amesema mwili huo umepatikana katika makutano ya mto Luiche na Ziwa Tanganyika, ambapo timu ya ukoaji imeuchukua mwili huo na kuupeleka katika Hospital ya rufaa ya mkoa Maweni kwa ajili ya taratibu nyingine.

Kupatikana kwa mwili huo kumekamilisha zoezi la kuwapata watoto wote wanne waliosombwa na maji tarehe ishirini na nne mwezi wa pili, baada ya mtumbwi waliokuwa wanautumia kuvuka kupinduka.

Kutokana na ajali hiyo ,Serikali ya mkoa wa Kigoma kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye, imegharamia shughuli za misiba ya watoto hao.