
Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt.Abubakar Zubeir Bin Ally ametuma salamu za pole kwa kanisa katoliki nchini pamoja na waumini wake, kufuatia tukio la uvamizi wa Kanisa Kuu la Kiaskofu, Jimbo la Geita, lililotokea hivi karibuni, ambapo ameitaka jamii kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwani vinasababisha uvunjifu wa amani ndani ya nchi.
.
Salamu hizo za pole zimewasilishwa na mwakilishi wa wake, ambaye ni Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke, baada ya kutembelea kanisa hilo na kujionea uvunjaji na uharibifu uliofanyika.
