Back to top

MUFTI : PINGENI KWA NGUVU, MAPENZI YA JINSIA MOJA

15 March 2023
Share

Mufti Mkuu wa Tanzania, Dkt.Abubakar Zubeir Bin Ally ,amesema ipo haja kama Taifa kuwa na mkakati wa pamoja wa kupambana  na tamaduni za kigeni zinazotweza utu, ikiwemo vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ,na kuwataka waisalam nchini kutumia mwezi mtukufu wa Ramadhan kupinga kwa nguvu vitendo hivyo ambavyo vimeanza kuenea kwa kasi nchini.