Back to top

Mume aua mke kwa kunyimwa unyumba kwa zaidi ya miaka miwili,Mara

08 May 2020
Share

Jeshi la polisi mkoa wa Mara limamshikilia Mokiri Wambura (46) mkazi wa Kengesi wilaya ya Serengeti mkoani Mara kwa tuhuma za kumuua mke wake Mwise Kyobe(38)  kwa kumkata mapanga na kisha kumuunguza kwa moto ndani ya nyumba  kwa madai ya kunyimwa tendo la ndoa kwa zaidi ya miaka miwili huku akimjeruhi kwa kumkata mapanga mtoto wake wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja.