
Kituo cha Runinga cha East Africa, kimezindua rasmi kampeni yake ya 'MWANAMKE KINARA' kwa mwaka 2023, ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka yenye lengo la kuwainua wanawake katika nyanja mbalimbali za kiuchumi.
Uzinduzi wa kampeni hiyo ambao umefanyika, mkoani Dar es Salaam, na imehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na binafsi.
Kwa mwaka huu wa 2023 kampeni hiyo imekuja na kauli mbiu isemayo 'MWANAMKE KINARA NGUVU ZAIDI' ikilenga kumkumbusha kila mwanamke kutambua mchango wake katika jamii.

Kwa mwaka 2022 kampeni ya Mwanamke Kinara ilifanya vizuri ikiwapa nafasi wanawake 10 wajasiriamali ambao hadi sasa wametambulika katika nyanja za kibiashara kwenye sekta mbali mbali kwa kujikwamua kibiashara na kiuchumi.
Kampeni ya 'Mwanamke Kinara' ya East Africa Television na East Africa Radio huzinduliwa mwezi wa tatu kila mwaka ikilenga kufungua milango kwa wanawake kiuchumi.


