
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Nnauye, amelaani tukio la waandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi, kushambuliwa na kujeruhiwa na kundi la vijana, wakati wakitimiza majukumu yao, katika eneo la uwanja wa Buriaga, mkoani Dar es Salaam.
.
Nape ameyasema hayo kupitia mtandao wa Twitter huku akibainisha kuwa anaamini vyombo vya dola, vitachukua hatua zinazostahili, kwani hadhani kama ni ngumu kuwapata waliofanya tukio hilo.