Back to top

NAPE ATANGAZA KIAMA KWA MATAPELI MTANDAONI

19 May 2023
Share


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Nnauye, ametangaza kiama kwa matapeli wa mtandaoni, kutokana na kuendelea kuwepo kwa vitendo hivyo vinavyosumbua wananchi.

Waziri Nape ametangaza kiama hicho, wakati akijibu hoja za wabunge waliotaka serikali kudhitibi uhalifu wa mtandao wakati wakichangia bajeti ya wizara ya habari.

Akiwasilisha bajeti ya wizara yake ya yenye shilingi zaidi ya milioni 212 ,Mhe.Nape Nnauyepamoja na mambo mengine amesema, katika mwaka ujao wa fedha, watafanya mapitio ya sera ya habari na utangazaji ili tasnia ya habari isimamiwe na sheria moja.

Kwa upande wa wabunge, wamechangia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuboresha mawasiliano na kuyumba kwa uchumi kwa vyombo vya habari.

Nayo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya miundombinu pamoja na mambo mengine imeitaka serikali kushusha gharama za mawasiliano.