Back to top

NASA YATANGAZA WANAANGA WATAKAOKWENDA MWEZINI MWAKA 2024

03 April 2023
Share

Shirika la Anga za Juu la Marekani (NASA), limetangaza wanaanga wanne, watakaokwenda mwezini, baada ya miaka 50 ya safari kama hiyo.
.
Safari hiyo ilyopewa jina la Artemis II mission, inayotarajiwa kuanza Novemba 2024 itajumuisha wanaanga wanne ambao ni Victor Glover, Christina Koch, Reid Wiseman na Jeremy Hansen.
.
Christina Koch atakuwa mwanaanga mwanamke wa kwanza kuwahi kutumwa kwenye safari ya mwezini, na Victor Glover atakuwa mwanaanga wa kwanza mweusi kwenye safari hiyo.

Koch, Glover (wanyuma) Hansen na Wiseman (waliokaa) 


Reid Wiseman (47): Rubani wa Jeshi la Wanamaji la Marekani ambaye amewahi kuhudumu kwa muda kama Mkuu wa Ofisi ya Mwanaanga ya NASA, pia amewahi kusafiri kwenda Kituo cha Anga cha Kimataifa (International Space Station) mwaka wa 2015.
.
Victor Glover (46): Rubani wa majaribio ya Jeshi la Wanamaji la Marekani ambaye alijiunga na NASA mwaka wa 2013 na kufanya safari yake ya kwanza ya anga mnamo 2020, Alikuwa Mwafrika wa kwanza kukaa kwenye Kituo cha Anga cha Kimataifa kwa muda mrefu (miezi 6).
.
Christina Koch (43): Ni Mhandisi wa umeme ambaye anashikilia rekodi ya kuwa mwanamke aliyekaa muda mrefu zaidi angani (siku 328).
.
Jeremy Hanson (47): Kabla ya kujiunga na Shirika la Anga la Kanada, alikuwa Rubani wa ndege za kivita wa Jeshi la Anga la Kanada.