
Maonesho makubwa ya bidhaa za maziwa ya yanayotajiwa kushirikisha zaidi ya makampuni arobaini kutoka nchi nane dunia yanatarajiwa kuanza kesho kwenye viwanja vyua themi jijiji Arusha huku takwimu zikionesha kuwa idadi ya unywaji wa maziwa kwa watanzania upo chini ukilinganisha na takwimu za kimataifa.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya maziwa nchini Lucas Malunde ametoa kauli hiyo kwenye kikao cha utangulizi kuelekea maadhimisho ya wiki ya unywaji wa maziwa inayotarajiwa kuanza wiki hii kwenye viwanja vya themi jijini arusha.
Mkurugenzi wa sera utetezi na mipango kutoka bazara la kilimo Tanzania Timoth Mbaga anasema lengo la maonesho hayo ni kuwawezesha wafugaji kupata elimu ya teknolojia ya kisasa katika ufugaji huku mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daquaro akieleza namna seerikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuwezesha uwekezaji wa kisasa katika sekta ya mifugo ikiwemo maziwa.