
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema utoaji huduma kupitia mtandao sio tu unaongeza ufanisi lakini pia unaongeza uwazi.
Mhe. Ndejembi ameyasema hayo baada ya kupatiwa maelezo ya huduma ya PSSSF Kidigitali, ambapo mwanachama kupitia Application ya PSSSF Kiganjani Mobile App, anaweza kupata taarifa zote zinazohusiana na uanachama wake katika Mfuko, wakati alipotembeela banda la PSSSF kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam, kwenye Viwanja vya Julius Nyerere, jijini Dar Es Salaam.