Back to top

NGAHOKORA WAPATE UMEME KABLA YA DESEMBA

19 September 2023
Share

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama, ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kuhakikisha linafikisha huduma ya umeme katika Kijiji cha Ngahokora kufikia mwezi Desemba mwaka huu.
.
Mhe. Jenista ametoa agizo hilo mara baada ya kuzindua  madarasa ya mfano ya Elimu ya Awali katika Shule ya Msingi Ngahokora iliyopo Kata ya Kizuka, Kijiji cha Ngahokora, Wilaya ya Songea Vijijini ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma.
.
Ameeleza kuwa kufikishwa huduma hiyo muhimu itakuwa mkombozi kwa wakazi wa eneo hilo katika kujikwamua kiuchumi kwa sababu utasaidia katika shughuli za uzalishaji na matumizi ya nyumbani pamoja kusaidia katika huduma za afya pindi wananchi wanapoenda kupatiwa matibabu katika Zahanati na Vituo vya afya.