
Watu kumi na tano wa familia saba, wamenusurika kifo baada ya nyumba wanayoishi katika mtaa wa Majengo ya zamani mjini Shinyanga, jirani na Msikiti wa Ijumaa wa Mufti Issa Simba, kuungua moto usiku wa kuamkia leo na kuteketeza baadhi ya mali zao.
ITV imefika katika tukio hili majira ya saa nne usiku na kushuhudia wananchi wakishirikiana bega kwa bega kuzima moto na kuokoa mali zilizokuwa ndani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishina Msaidizi wa Polisi Janeth Magomi, amethibitisha kutokea tukio hilo na kuwaopongeza vijana na majirani wa mtaa huo, kusaidiana bega kwa bega kuzima moto huo huku akiwashauri wananchi kuhakikisha wanakuwa na vizimia moto kwenye nyumba zao.