Back to top

ODINGA ADAI KULIKUWA NA JARIBIO LA KUMUUA

21 March 2023
Share

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amedai kuwa kulikuwa na jaribio la kumuua yeye na Kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka wakati wakiongoza maandamano ya kulalamikia gharama za maisha nchini humo na kufunguliwa kwa server za uchaguzi mkuu uliopita, yaliyofanyika jana Machi 20, 2023, Jijini Nairobi.
.
Odinga amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amebainisha kuwa magari yaliyokuwa yamewabeba yalipigwa risasi kwenye maandamano hayo.