
Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Prof.Joseph Msambichaka amesema uamuzi wa serikali kupitia TAEC kujenga ofisi na maabara Zanzibar kutasaidia kusogeza huduma ya upimaji wa mionzi karibu na wananchi.
Prof. Msambichaka ameyasema hayo baada ya kutembelea ofisi na maabaza za TAEC Zanzibar zilizojengwa eneo maalum lililotengwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Aidha Prof. Msambichaka amesisitiza kuwa zamani ilibidi kubeba sampuli kutoka Zanzibar kupeleka Arusha au Dar es salaam kwa ajili upimaji wa mionzi jambo ambalo liligharimu fedha Pamoja na muda ili kupata majibu ambapo kwa sasa upimaji utafanyika Zanzibar jambo litakalosaidia kukuza Uchumi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Prof. Najat Kassim Mohammed ameishukuru serikali kwa kutoa eneo la ofisi na maabara za TAEC ni jambo ambalo litasaidia kuhakikisha matumizi salama ya mionzi nchini.
