Back to top

Ofisi ya mkemia yatahadharisha kuhusu matumizi ya kemikali nchini.

25 February 2020
Share

Mkemia Mkuu wa serikali Dk Fidelice Mafumiko amesema ofisi yake haitamvulia mtu yoyote ambaye atabainika kutumia ama kuingiza kemikali nchini bila ya kufuata sheria na taratibu zilizopo  kwani madhara ya kemikali yanagusa kizazi hadi kizazi.

Dk Mafumiko ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati alipokutaka na watumiaji wa  kemikali hizo nan kutawadharisha kuwa lazima  wawe makini wakati wanapozitumia.

Naye Mkurugenzi wa idara ya  usimamizi na udhibiti wa kemikali Daniel ndio amesema sheria ipo wazi kuwa mtumiami wa kemikali lazima awe na kibali.

Baadhi ya watumiaji wa kemikali hizo hivyo wamesema wanatambua umuhimu wa kuzitumia na uangalifu japo  wanatakiwa kupewa taarifa za mara kwa mara.