Back to top

Ouattara aidhinishwa kuwania tena kiti cha urais.

15 September 2020
Share

Nchini Côte d'Ivoire, Mahakama ya Katiba imemuidhinisha rais anayemaliza muda wake Alassane Ouattara kuwania kwenye kiti cha urais katika uchaguzi wa urais kwa muhula mwingine Guillaume Soro na Laurent Gbagbo hawakuidhinishwa.

Faili 44 zilikuwa zimewasilishwa kwa Mahakama ya Katiba, lakini mahakama hiyo imepitisha nne na ndizo zimepokelewa ikiwa ni pamoja na ile ya Rais Ouattara.

Wagombea wengine wa Urais waliopitishwa ni wa Chama cha PDCI Henry Konan Bédié , Mgombea wa chama cha SPI Pascal Affi N'Guessan, na Kouadio Konan Bertin anayejulikana zaidi kwa herufi za mwanzo za majina yake KKB, aliyejitenga na chama cha PDCI.

Siku ya Jumapili kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro aliteuliwa kupeperusha bendera ya chama chake katika uchaguzi wa urais wa mwezi Oktoba.