
Baada ya sakata la aliyekuwa mchezaji wa Yanga SC Feisal Salum kumalizika kwa kununuliwa na timu ya Azam FC, mchezaji huyo amesema pesa zote ambazo aliomba kuchangiwa ili apeleke sakata lake CAS, atazipeleka kwa watoto yatima, msikitini na kanisani, ambapo amedai kuwa anafanya hivyo kwani pesa si haki yake na ni ngumu kujua nani alituma.
