Back to top

Polisi Geita wakanusha upendeleo wa ulinzi mikutano ya kampeni.

15 October 2020
Share

Jeshi la polisi mkoani Geita limekanusha taarifa za kuwepo kwa upendeleo wa ulinzi katika mikutano ya kampeni ya  vyama vya siasa  na kupendelea baadhi ya vyama kwa kusema kuwa vyama vyote vinapewa ulinzi sawa bila upendeleo hata kama mkutano una watu wawili.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe anasema wamekuwa wakitoa ulinzi sawa kwa vyama vyote huku akiwataka wagombea ubunge na udiwani kufanya kampeni kwa kufuata muda uliowekwa na tume ili kuepuka vurugu na kushambuliana kwa mawe.