Back to top

Polisi Ruvuma yakamata mizani ya NFRA na vifaa vya TANESCO vilivyoibwa

09 June 2021
Share

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanya operesheni mkoani humo na kufanikiwa kukamata vifaa mbalimbali vilivyoibwa ikiwemo mizani miwili ya Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) kanda ya Songea na vifaa vya umeme mali ya shirika la TANESCO.


Kaimu Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Pili Mande amesema vifaa vingine vilivyokamatwa ni TV, lita 80 za gongo na mali mbalimbali za wizi pamoja na watuhumiwa saba wa wizi ikiwemo mali za TANESCO na NFRA na wengine kukutwa na gongo ambapo thamani ya vifaa vilivyoibwa bado haijajulikana.
.
Aidha, katika hatua nyingine Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanya operesheni ya kukamata waendesha bodaboda wasiofuata sheria na bodaboda zao ambapo waendesha bodaboda 110 na abiria 67 wamekamatwa.