
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Camillus Wambura, amesema askari wa Jeshi hilo wanatarajia kupata mafunzo nchini Korea, ambapo amebainisha kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano baina ya Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Serikali ya Korea (KOICA) na Jeshi la Polisi Tanzania.
.
IGP Wambura ameyasema hayo wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano wa miaka mitatu, ambapo amesema kupitia mafunzo hayo Askari hao watapata mafunzo mbalimbali yakiwemo ya upelelezi wa makosa ya kimtandao, upelelezi wa makosa ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia na uchunguzi wa kisayansi.