Back to top

POLISI WAWILI NA KARANI WA MAHAKAMA WAFA AJALINI

05 March 2023
Share

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Ndwanga Dastani miaka 28,  Konstebo Emmiliana Charlse miaka 26 Askari wa Kituo cha Polisi Chalinze na Karimu Simba miaka 27, Karani wa Mahakama ya Wilaya ya Lugoba wamefariki dunia baada gari lenye namba za usajili T.323 BAL aina ya Toyota Crester lililokuwa likiendeshwa na Ndwanga Dastani, kuacha njia na kugonga karavati kisha kupinduka katika maeneo ya Mavi ya Ng'ombe, Kijiji cha Mboga, Tarafa ya Chalinze, mkoani wa Pwani, katika barabara ya Chalinze/Segera na kusababisha vifo vya watu hao na majeruhi mmoja.