Back to top

Profesa Lipumba atoa ahadi ya kuongeza mzunguko wa fedha.

25 September 2020
Share

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba akiwa mkoani Kagera ameahidi kuwa endapo wananchi watamchagua na kumpa mamlaka ya kuingia Ikulu serikali ya chama hicho itahakikisha inaongeza mzunguko wa  fedha ili kila mwananchi aweze kutimiza adhima yake ya kujiletea maendeleo.  
 
Profesa Lipumba ambaye amepata mapokezi makubwa kutoka kwa wananchi wa Katoro, ametoa ahadi hiyo kwa nyakati tofauti kwenye mikutano yake ya kampeni ya kunadi sera za chama hicho iliyofanyika Bukoba vijijini kwenye maeneo ya Kasharu, Ntoma, Katerero, Kyema na Mugaza pamoja na Butelankuzi, amesema dhamira yake kubwa ni kulainisha vyuma vilivyokaza. 
 
Mgombea huyo amesema endapo atachaguliwa atahakikisha anatafuta soko la uhakika la kahawa inayozalishwa na wakulima wa walioko mkoani Kagera ambao amedai wanalipwa bei ambayo hailingani na nguvu wanayoitumia kuizalisha.