
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Prof.Azaveri Lwaitama ameieleza Mahakama kuwa Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee na wenzake 18 wakitoka bungeni leo yeye atakuwa mtu kwa kwanza kuwatetea ili warudishwe kwenye chama hicho, na kufuata utaratibu wa kurudi tena bungeni.
.
Prof.Lwaitama amedai hayo March 10, mbele Jaji Cyprian Mkeha wa Mahakama Kuu, Masjala Kuu Dar es Salaam, wakati akijibu maswali ya dodoso, kutoka kwa Wakili wa waleta maombi, Ipilinga Panya yaliyotokana na kuchezwa kwa video iliyomuonesha Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe akizungumza.
.
Mjumbe huyo, alidai Mbowe alikuwa akizungumza kwamba, alimuita Mdee Jijini Nairobi, nchini Kenya ili kuzungumza nae kwa kile ambacho wamekifanya kwa sababu yeye ndiyo alikuwa kiongozi wa wenzie kutokana na ushawishi mkubwa aliyokuwa nao.
