Back to top

Rais Dkt.Magufuli kufanya ziara ya kikazi ya siku nane Mbeya

24 April 2019
Share

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwasili mkoani mbeya kesho kwa ajili ya kuanza ziara ya siku nane mkoani humo ambapo atashiriki misa ya kusimikwa kwa askofu mkuu wa jimbo katoliki la Mbeya, kukagua miradi, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo kwenye wilaya nne za mkoa wa Mbeya.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema rais Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli atawasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya  majira ya saa 10 jioni na kuelekea ikulu ndogo kwa shughuli za kiserikali na siku inayofuata ataanza kutembelea miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi wa jiji la Mbeya.

Mkuu huyo wa mkoa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea na kumsikiliza rais wao huku akiwataka kutumia ziara hiyo ya rais kama fursa ya maendeleo na kubeba mabango yenye ujumbe unaoonyesha kero zao badala ya kuandika mabago ya uchochezi.