Back to top

Rais Magufuli amteua Prof. Shukrani Manya kuwa Naibu Waziri Madini.

11 December 2020
Share

Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Shukrani E. Manya kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Prof. Manya pia ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Manya alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Tanzania.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano IKULU imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Manya unaanza leo tarehe 11 Desemba, 2020 na ataapishwa leo mchana Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma.