Back to top

RAIS MUSEVENI AKUTWA NA MAAMBUKIZI UVIKO-19

08 June 2023
Share

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekutwa na maambukizi ya Uviko-19, ambapo Katibu wa kudumu wa Wizara ya afya nchini humo, Diana Atwine, amesema Rais Museveni alipata dalili za mafua lakini yuko katika hali nzuri na ataendelea na majukumu yake na atafuata taratibu za kawaida za kuzuia maambukizi ya Uviko-19 wakati akitekeleza majukumu yake.
.
Uganda ilikuwa moja ya baadhi ya nchi za barani Afrika zilizochukua hatua kali kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo, wakati wa janga hilo, ikiwa ni pamoja na kutekeleza amri ya kutotoka nje kwa muda mrefu na kufungwa kwa shule na biashara.