
Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Samia Suluhu Hassan, amewaapisha Mawaziri watatu aliowateua katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri aliyofanya.
Walioapishwa katika Ikulu ya Dar es Salaam ni Mhe.Angellah Kairuki kuwa waziri wa TAMISEMI, Mhe.Stergomena Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe.Innocent Bashungwa kuwa waziri wa ulinzi.

Akiongea baada ya kuapishwa Mawaziri hao Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka kuzingatia kiapo chao cha kulinda kuihifadhi na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano, kutokutoa siri za Baraza la Mawaziri na kuheshimu mipaka yao ya kazi kwa mujibu wa mamlaka waliyopewa.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Tanzania Mhe.Tulia Ackson amesema tayari amemwapisha Mhe. Angellah Kairuki, kuwa mbunge kabla ya kufika Ikulu kwa kiapo cha nafasi ya Waziri wa TAMISEMI.
