Back to top

RAIS SAMIA AMETOA MCHANGO USHINDI WA PROF.JANABI

21 May 2025
Share

Naibu Mwakilishi wa Kudumu Tanzania-Geneva, Balozi Hoyce Temu ambaye alikuwa kwenye Timu ya kampeni ambayo ilizunguka Mataifa mbalimbali kumuombea kura Prof. Janabi kwenye nafasi ya Mkurugenzi wa WHO- Africa,  amesema Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu ametoa mchango mkubwa uliowezesha ushindi wa Janabi.

Kupitia taarifa aliyoitoa, Hoyce amesema "MAMA, kama tupendavyo kumwita, amefanya mengi sana, huenda wapo ambao wanaweza kudhani kuwa kwavile hakuwa na sisi, basi hakushiriki kikamilifu, la hasha, Mama alifanya mengi, mtaani tungesema ameupiga mwingi”

“Mama ameonesha umakini kwa kumteua Mtu makini, Prof. Janabi, kugombea nafasi hiyo, ukiwa na Mgombea mwenye sifa hata ugumu wa kampeni hupungua, pili Mama aliunda timu ya kampeni iliyokuwa na Wajumbe wenye uwezo mkubwa, Timu nzuri ya kampeni hurahisisha ushindi.

“Tatu, alimteua Rais Mstaafu, Mhe Jakaya Kikwete, kuwa Mwenyekiti wa kampeni, hii pia ilionesha jinsi MAMA alivyo makini, kuwepo kwa Mhe Kikwete kama Mwenyekiti kulikuwa ni chachu kubwa kutokana na uzoefu wake, nakumbuka tukiwa Gambia, Rais Adama Barrow alisema kwa utani kuwa si rahisi kuona Marais wawili wakifanya kazi pamoja!, hii inaakisi ukweli kuwa Mama aliteua timu makini kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa lake”

“Nne, Mama alionesha uongozi imara muda wote wa kampeni, daima alikuwa alikuwa akitoa miongozo kupitia Mawaziri, Mhe Mohamoud Thabit Kombo na Mhe Jenisfter Mhagama, sikumbuji kama kuna siku ilipita bila kupata updates toka kwake kupitia Mwenyekiti na hata Mawaziri hao, alifuatilia kwa karibu kila hatua tuliyokuwa tunapiga na kila tulipoweka mguu, alijua tukichokuwa tunafanya, palipokuwa panajitokeza changamoto, alikuwa mstari wa mbele kurekebisha kwa kutumia njia zake kwani Kiongozi mzuri ni yule mwenye mbinu anuai za kutatua changamoto. 

“Sita, Utashi au Political will ya Mama kwenye kupigania suala lenye maslahi ya Taifa ulikuwa mkubwa sana, na hii haikuwa mara ya kwanza kwani sote tumeshuhudia kwenye chaguzi nyingine mf. Mhe Dr. Tulia Ackson alipokuwa akigombea kuwa Rais wa Mabunge ya dunia, Mama pia alitoa mchango mkubwa sana na alifanikisha ushindi wa Ndugulile, huyo ndiye Mama Samia Suluhu Hassan, Mwanadiplomasia Namba Moja nchini.”