Back to top

Rais Samia awatakia Watanzania Pasaka Njema na kuliombea Taifa Amani.

04 April 2021
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais .Samia Suluhu Hassan amewatakia Watanzania wote Pasaka Njema, huku akisisitiza Amani, Upendo na Mshikamano.

Kupitia Taarifa aliyoiandika kupitia ukurasa wake wa Twitter ameongeza kwa kuwataka Watanzania kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa.

"Nawatakia watanzania wote Pasaka njema, tuadhimishe ufufuko wa Yesu Kristo huku tukiliombea Taifa letu la Tanzania kudumisha amani, upendo na mshikamano. Tuendeleze jitihada za kuijenga nchi yetu kwa kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa"-Mhe . Rais Samia Suluhu.

Yesu amefufuka, Haleluya Haleluya.
Rais Samia awatakia Watanzania Pasaka Njema na kuliombea Taifa.