
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan, amekubali kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ulioandaliwa na Baraza la Wanawake la chama hicho (BAWACHA) utakaofanyika Machi 8, 2023, mkoani Kilimanjaro.