
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amekataa ombi la Gavana wa Gauteng, Panyaza Lesufi, alilokuwa amemuandikia Rais huyo, akiomba ruhusa ya kumfanyia mazishi ya kitaifa rapa Kiernan Forbes, maarufu kama AKA, aliyeuawa kwa kupigwa risasi, hivi karibuni nchini humo.
.
Akizungumza kupitia vyombo vya habari nchini humo, Gavana huyo alibainisha kuwa hakuomba fedha za serikali kwa ajili ya mazishi, bali jeneza lifunikwe bendera ya Taifa na ipeperushwe nusu mlingoti kwa heshima ya rapa huyo.