Back to top

RC SENDIGA ATOA SIKU 7 UJENZI KITUO CHA AFYA KIKAMILIKE RUKWA

08 January 2023
Share

Wananchi katika kata ya Samazi wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa kituo cha afya Samazi, kutokana na ujenzi wake kuchukua muda zaidi ya miaka 5 bila kukamilika.

Hatua hiyo imesababisha akinamama wajawazito kulazimika kujifungulia watoto njiani, kutokana na vituo vya afya vilivyopo kuwa umbali wa zaidi ya kilomita 50 kutoka maeneo wanayoishi kwa sasa.

Wameyasema hayo kupitia mkutao wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Samazi na kuiomba serikali kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya Samazi ili kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu wakati wa kutafuta huduma za matibabu.

Hali hiyo imefanya mkuu wa mkoa wa mkoa wa Rukwa Queen Sendiga, kuingilia kati na kuagiza uongozi wa Halmashauri hiyo kukamilisha ujenzi huo ndani ya siku 7 na kituo hicho kikamilishwe na kuanza kutoa huduma ya afya kwa wananchi.