Back to top

SAMIA ARIDHIA KUJIUZULU KWA KINANA CCM

29 July 2024
Share

 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amejiuzulu wadhifa huo baada ya Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuridhia ombi lake.

Taarifa ya kujiuzulu kwa Kinana imebainishwa kwenye taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Bw. Amos Makala, akisema Kinana ameandika barua ya kuomba kupumzika.

Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema "Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako." Imesema taarifa hiyo.

Pia Dkt. Samia amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Kinana kila itakapohitajika.