Back to top

SANDF MAZOEZI YA PAMOJA URUSI NA CHINA

20 January 2023
Share

Jeshi la Afrika Kusini limetangaza kuwa mwezi ujao litafanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Urusi na China katika maeneo ya pwani yake.

Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Kitaifa la Afrika Kusini (SANDF) wamesema lengo la mazoezi hayo ni kubadilishana ujuzi na maarifa ya kiutendaji. 

Mazoezi hayo yatafanyika kwa siku 10 kuanzia tarehe 17 Februari hadi 27 Februari katika mji wa bandari wa Durban na Richards Bay.

Afrika Kusini ilikuwa miongoni mwa nchi za Kiafrika ambazo zilijiepusha na kuunga mkono uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.