Back to top

SERIKALI HAITAKOPA ILI KULIPA MISHAHARA - RUTO

12 April 2023
Share

Rais wa Kenya, William Ruto amekiri kuwa serikali yake inakabiliwa na changamoto ya kuchelewesha kulipa mishahara kwa wafanyakazi wa umma, ambapo amedai hali hiyo imesababishwa na madeni makubwa yanayoikumba nchi hiyo.
.
Rais Ruto ameshikilia kuwa serikali hiyo haitakopa ili kulipa mishahara badala yake inapania kupunguza matumizi ya fedha, kauli ambayo imeonekana kuwa kinyume na Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ya nchi hiyo, ambayo imebaini kuwa serikali ya Rais huyo imekopa shillingi Bil. 500 za Kenya katika siku 120 zilizopita.