
Serikali imepanga kuajiri wataalamu wa afya 12,000, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha huduma kwa wananchi hasa maeneo yenye upungufu wa watumishi hao ambapo hatua hiyo itapunguza changamoto ya ajira kwa wataalamu wa afya nchini.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Bungeni, Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mhe. Minza Simon Mjika.
.
Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amesema, wataendelea kuwapanga watumishi kwenye mikoa ya pembezoni mwa nchi, kutokana na unyeti wa mikoa hiyo kupakana na nchi nyingine hasa zenye milipuko ya magonjwa.
