Back to top

Serikali kufanayia tahmini vyama vyama vya ushirika kuepusha udalali.

10 September 2019
Share

Serikali imesema inafanya tathimini kupitia mfumo mzima wa ushirika kwa kuangalia muundo wake, uendeshaji na usimamizi wa rasilimali zake pamoja na fedha za wanachama ili kuleta tija katika  kufanya biashara zaidi kuliko udalali ulipo sasa.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Omari Mgumba wakati akijibu swali la Mhe.Amina Makilagi mbunge wa viti maalum aliyeuliza serikali ina mkakati gani kuhakisha vyombo   vya ushirika vinaimarika.

Mhe.Mgumba akasema kuwa wizara kupitia tume imeendelea kuimarisha misingi ya utawala bora na uwajibikaji katika vyama vya ushirika kwa kufanya kaguzi za mara kwa mara yaani mara mbili kwa mwaka.

Akaongeza kuwa mikakati mingine ni pamoja na kuhamasisha wadau mbalimbali hususani vijana, wanawake na vikundi vyenye mwelekeo wa ushirika kujiunga ama kuanzisha vyama vya ushirika vya akiba.

Mhe.Mgumba akaongeza kuwa vikianzishwa vyama vya ushirika vya akiba na mikopo yaani SACCOS kwenye vyama vya ushirika vya kilimo na masoko yani AMCOS vitawajenga wakulima tabia ya kuweka  akiba na kupata mikopo yenye masharti nafuu.