
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha za kununua magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) 727 yatakayotumika kutoa huduma kwenye hospitali za rufaa nchini.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, wakati akijibu swali la Mbunge wa Nyasa, Mhe. Stella Manyanya katika Mkutano wa kumi kikao cha nane, Bungeni Jijini Dodoma.
.
Aidha, katika kuboresha hospitali ya Rufaa ya kanda ya kusini, tayari Serikali imetoa jumla ya shilingi Bilioni 4.4 itayosaidia kujenga majengo ya nyumba za wafanyakazi, ujenzi wa chumba cha kuhufadhia maiti, umaliziaji wa maabara na umaliziaji wa jengo la mama na mtoto.
.
Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amesema, Serikali inaendelea kuboresha huduma nchini, na tayari Serikali imeanza kupeleka madaktari bingwa katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya kusini, huku vifaa kama CT-SCAN pamoja na MRI vikiwa tayari vimefungwa tayari kuanza kutoa huduma.
