Back to top

SERIKALI NA WADAU WASAIDIE WATOTO KUTUMIA MABADILIKO YA DIGITAL

09 May 2022
Share

Umoja wa Mameneja na wamiliki wa shule na vyuo visivyo vya serikali nchini (TAMONGSCO) umeiomba serikali pamoja na watalaam mbali mbali wa elimu kushirikiana ili kuwawezesha watoto kuweza kutumia vizuri mabadiliko ya Digital kwa kuyageuza mabadiliko hayo kuwa uwanja mzuri wa kujifunzi na kupanua uwanja watoto kujisomea ilikusiwepo na mtoto ananyeachwa nyuma.

Akielezea wakati akiendesha mashindano ya chemsha bongo baina ya shule 10 Jijini Dar es Salaam ikiwa kama sehemu ya kuendeleza utamaduni wa kujisomea na kujiendeleza katika elimu, Mwenyekiti wa Taifa wa (TAMONGSCO) Alfred Luvanda amesema uwepo wa majukwa ya Kidijital yenye kutoa fursa kwa watoto kuweza kujisomea masomo mbali ya shuleni kwa njia ya Kidijita ikiwemo jukwa la TESEA ni hatua muhimu ya kuungana na wengine kuwasilisha suluhu zinazo unganishwa na Teknolojia ilikusiwe na mtoto hatakayeachwa nyuma kwa kuhakikisha kila Mwanafunzi anapata nyenzo za kujifunzia kupitia majukwa ya Kidijitali sanjari na mataifa mengine duniani ili kulifanya taifa kunufaika na maendeleo hayo ya Teknolojia.

Aidha kwa pande kwa upande wa Mkurugenzi wa  Digital Academia Limited (DATL) Mombokaleo amesema muda wa sasa kwenye sekta ya elimu ni kujikita kwenye Digital kwani hiyo ndio njia peke inaweza kumuhakikishia kila mwanafunzi wa Kitanzania kupata nyezo zote za kujifunzia kwenye ncha za mikono yake nyezo zilizo sawa na mtaala wa taifa wa elimu na kuwafanya watoto kuwa na matumizi mazuri ya mabadiliko ya  Kigigital.