
Serikali ya Kenya imesema inahitaji angalau miaka miwili kufufua uchumi wa nchi hiyo, na Wakenya wanapaswa kujipanga kukabiliana na ugumu wa maisha.
Waziri Mkuu wa Kenya Bwana Musalia Mudavadi, amesema hayo bungeni wakati akijibu maswali kuhusu jitihada za serikali za kupunguza gharama za bidhaa za msingi.
Amesema serikali haina uwezo wa kudhibiti sababu zinazochangia gharama za juu za maisha, na nchi iko katika matatizo ya kiuchumi ya muda mrefu.
Aidha, ametaja mkakati wa muda mfupi wa kuwalinda raia wa Kenya dhidi ya hali mbaya ya uchumi, kuwa ni pamoja na kuondoa ushuru wa bidhaa za chakula kutoka nje ya nchi, kupunguza uagizaji wa mazao kutoka nje na kupanda mazao yanayostahimili ukame na kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo.
